Ghana’s Communications Minister, Sam George, has released photos of a Russian citizen who secretly recorded and published intimate photos of Ghanaian women. The man is accused of using hidden camera glasses to film sexual encounters without consent, with authorities initiating extradition and legal action
The country is following up on the matter to ensure he is brought to justice.
Ghana’s Foreign Minister called the Russian ambassador to the country and it was reported that the two countries “are working together to track the person.”
At a press conference in Accra, the minister of communication Samuel George printed the man’s passport, which had the name of Vladislav Liukov.
Samuel George said: “wizara za mawasiliano na jinsia zinamjua bwana huyu ni nani na pasipoti yake aliyoingia nayo nchini.”
Amesema baadhi ya wanawake wamewasilisha malalamiko rasmi ambayo yatawasilishwa katika ofisi ya mwanasheria mkuu kwa hatua.
Amesema “polisi pamoja na mamlaka ya usalama wa mtandao watalipeleka suala hilo kwa Interpol kutoa hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa bwana huyo.”
Waziri huyo pia amesema mamlaka ya usalama wa mtandao ambayo imeendesha uchunguzi kuhusu suala hili inajiandaa kumshtaki mshukiwa hayupo.
Waghana wengi wanataka mshukiwa akamatwe huku baadhi ya watu wanasema waathiriwa walikubali wenyewe.
Waziri wa jinsia wa Ghana Agness Naa Momo Lartey amesema “sio wanawake wote ambao picha zao zilichapishwa kwenye mitandao ya kijamii walikutana kimapenzi na mshukiwa.”
Alisema “baadhi ya wanawake hawa wanajiua hasa wale ambao hawakuwa na uhusiano wa kimapenzi na mshukiwa.”
Agnes Naa Momo Lartey anataka waathiriwa waonewe huruma huku wizara yake ikiendelea kuwapa msaada wa kisaikolojia wale waliojitokeza.
Uchunguzi wa awali uliofanywa na mamlaka ya usalama wa mtandao umebaini kuwa mshukiwa alirekodi matukio ya kimapenzi na baadhi ya wanawake na kujipatia pesa kupitia majukwaa ya mtandaoni.
Sheria ya usalama wa mtandao ya Ghana, 2020 (Sheria ya 1038) inakataza kurekodi na kusambaza picha za kimapenzi bila ridhaa.
Mtu anayepatikana na hatia anaweza kukabiliwa na kifungo cha hadi miaka 25 jela.

